Takriban mimba zisizotarajiwa milioni 121 zilitokea kila mwaka kati ya 2015 na 2019. Zinapotumiwa kwa usahihi, kondomu za kike huwa na uwezo wa 95% katika kuzuia mimba na maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Kondomu za kiume (za nje) hutoa kizuizi kisichoweza kupenyeka kwa chembe chembe za magonjwa ya magonjwa ya zinaa na VVU na zina ufanisi wa 98% katika kuzuia mimba zinapotumiwa ipasavyo. Kondomu inasalia kuwa njia inayotumika zaidi ya kupanga uzazi miongoni mwa vijana na kutoa ulinzi dhidi ya mimba zisizotarajiwa, magonjwa ya zinaa na VVU.
Watu wengi husahau uwezo wa kondomu kama zana ya kupanga uzazi. Mkusanyiko huu unatukumbusha jinsi kondomu zinavyosalia kuwa muhimu hata uvumbuzi wa FP/RH unapoibuka.