Ingawa kuna watumiaji zaidi ya milioni 60 wa ziada wa uzazi wa mpango wa kisasa katika nchi zinazozingatia FP2020 ikilinganishwa na 2012, ajenda yetu bado haijakamilika, na taarifa na huduma bora za upangaji uzazi bado hazijawafikia wengi wa wale walio na uhitaji mkubwa zaidi. Ili kuwafikia wanawake, wasichana na wenzi wao kwa usawa, tunahitaji kujua ni nani anakabiliwa na tatizo kubwa zaidi.