Mitandao ya kijamii imezidi kuwa mojawapo ya maeneo maarufu kwa watu binafsi kutoa maoni yao na kushiriki katika mazungumzo kuhusu kile wanachokiona, kusikia na kuamini. Kwa sasa kuna watumiaji bilioni 3.4 wa mitandao ya kijamii, takwimu inayokadiriwa kuongezeka hadi bilioni 4.4 ifikapo 2025. Umaarufu huu unaoongezeka unamaanisha kuwa mitandao ya kijamii inaweza pia kuwa nyenzo muhimu ya kukusanya taarifa kuhusu afya ya uzazi na upangaji uzazi kwa hiari.