Mradi wa Twin-Bakhaw unatetea usawa wa kijinsia kupitia huduma za afya ya ngono na uzazi miongoni mwa watu wa kiasili. Kila mtoto mchanga atakuwa na mche “pacha” wa mikoko, ambao familia ya mtoto mchanga lazima iupande na kuutunza hadi ukue kabisa. Mradi unaonyesha umuhimu wa upangaji uzazi na afua za afya ya uzazi katika hatua za muda mrefu za ulinzi wa mazingira. Hii ni sehemu ya 2 ya 2.